Walimu na majaji waandamana Mexico siku 8 kabla ya kombe la dunia
Eric Buyanza
June 4, 2026
Share :

Siku 8 kabla ya Mexico City kuanza Kombe la Dunia, maandamano makubwa ya walimu na majaji waliostaafu yalisababisha kufungwa kwa barabara na kuleta fujo kubwa jana Jumatano kwenye mji huo.
Tarehe 11 Juni, jiji la Mexico litakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia kati ya Mexico na Afrika Kusini kwenye uwanja wa Azteca.
Waandamanaji hao wamesema maandamano yao hayahusiani na mashindano hayo, na yanaweza kushika kasi kama serikali ya Rais Claudia Sheinbaum haitashughulikia madai yao.
Muungano huo unaitaka serikali kutimiza ahadi ya kampeni ya kufuta sheria ya mwaka 2007 ambayo ilirekebisha mfumo wa pensheni na hifadhi ya jamii kwa wafanyikazi wa sekta ya umma, pamoja na nyongeza ya mishahara.





