Walinzi wa Rais wakamatwa kwa tuhuma za Uhaini
Sisti Herman
May 21, 2024
Share :
Baada ya kufeli kwa jaribio la tisa (9) la kumpindua Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore siku kadhaa zilizopita, vyombo vya habari vya kimataifa vimethibitisha kwamba jaribio hilo lilifanywa na mmoja wa walinzi wa Rais ambaye aliwafyatulia risasi walinzi wenzake.
Mara baada ya kumdhibiti mlinzi huyo, intelijensia ya Burkina Faso imewakamata walinzi wa Rais 12 kwa ajili ya mahojiano na upelelezi yakinifu kwa maana inasemekana waliuhusika kupanga uasi huo.