Waliofikisha miaka 25 na bado wanaishi kwa wazazi, sasa kutozwa kodi
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Huko nchini Kenya, muswada wa Fedha wa mwaka 2024 umeipa serikali mbinu mpya ya kukusanya mapato kutoka kwa vijana wenye umri wa zaidi ya miaka 25 ambao bado wanaishi kwa wazazi wao.
Muswada huo unapendekeza kwamba mtu yeyote aliyefikisha umri wa miaka 25 na bado anaishi kwa wazazi wake atachukuliwa kuwa yuko Kaya tofauti na ile ya wazazi.
"Mtu ambaye ametimiza umri wa miaka 25 na hana mapato yake mwenyewe au anaishi na mchangiaji atachukuliwa kama yuko Kaya tofauti na mchangiaji," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Hii itatumika pia kwa watu ambao hawajaajiriwa lakini wamefikia umri huo.
Pendekezo hilo linasema kuwa watu hao watahitajika kulipa KSh 300 kwa mwezi (sawa na shilingi 6,000 za kitanzania).
TUKO