Waliokuwa nje na Timu za Taifa, kurejea baada ya kuombewa ruhusa
Eric Buyanza
March 23, 2024
Share :
Wachezaji wa Simba, Aishi Manula, Hussein ‘Tshabalala’, Kibu Denis na beki Kennedy Juma waliokuwa na kikosi cha Taifa Stars iliyokuwa uwanjani jioni ya jana kucheza na Bulgaria wanaanza safari kurudi nyumbani kuja kuongeza nguvu katika kambi ya Simba iliyopo Zanzibar.
Saido ambaye yuko Madagascar na timu ya taifa ya Burundi, naye atawahi kabla ya mechi na Al-Ahly...“Nimeombewa ruhusa na klabu...nadhani nitarejea mapema na nitawahi maandalizi ya mwisho ya timu kabla ya mechi,” anasema Saido.
Chama, yupo Malawi akiwa na kikosi cha Zambia kitakachocheza leo jioni dhidi ya majirani zao Zimbabwe na baada ya hapo atapanda ndege kurejea kambini Zanzibar zikiwa zimesalia siku kama nne kabla ya mechi ya CAF.