Waliopanga njama za kumuua Zelensky wakamatwa
Eric Buyanza
May 8, 2024
Share :
Mamlaka za usalama nchini Ukraine zimesema zimebaini njama ya Urusi ya kufanya shambulizi dhidi ya Rais Volodymyr Zelensky na wanasiasa wengine wa nchi hiyo.
Shirika la Ujasusi la Ukraine, SBU, limesema maafisa wawili kutoka idara ya usalama inayohusika na ulinzi wa rais wamekamatwa kuhusiana na kushiriki mpango wa mashambulizi hayo.
Inaarifiwa maafisa hao walivujisha taarifa za siri kwa idara ya ujasusi ya Urusi kwa ahadi ya malipo ya fedha na wamekuwa wakiandaliwa kufanya hujuma dhidi ya rais Zelensky na maafisa wengine wa serikali ya Ukraine.
Taarifa ya SBU imesema waliokamatwa ni maafisa wenye vyeo vya ukanali. Inafahamika Urusi iliwahi kuwatuma makomandoo wake wa kijeshi mjini Kyiv kumkamata au kumuua rais Zelensky, hata hivyo mpango huo ulishindwa.