Waliopanga Ugaidi wa Sept 11, 2001, waingia makubaliano ya kukiri mashtaka ili kuepuka adhabu ya kifo
Eric Buyanza
August 1, 2024
Share :
Watu watatu wanaotuhumiwa kupanga na kuhusika moja kwa moja kwenye mashambulio ya kigaidi la Septemba 11, 2001 wameingia kwenye makubaliano ya kabla ya kesi ili kukiri mashtaka yanayowakabili, jambo litakalowawezesha kuepuka adhabu ya kifo iliyokuwa inakwenda kuwakabili.
Khalid Sheikh Mohammad, Walid Muhammad Salih Mubarak Bin Attash, na Mustafa Ahmed Adam al-Hawsawi wamezuiliwa katika kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani Guantanamo Bay, nchini Cuba, kwa miaka mingi bila kufikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, watu hao watakiri kuwa na hatia kwa makubaliano kuwa upande wa mashtaka ukubali kutowapa hukumu ya kifo.