pmbet

Walitufunga 3 sasa tupo kwao pointi 3 tunazitaka - Bakari

Eric Buyanza

April 2, 2025
Share :

Ni mechi ya kisasi!, ndivyo unaweza kusema wakati Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, watakaposhuka leo kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kujaribu kulipa kisasi dhidi ya Tabora United, huku wachezaji wa timu hiyo, wakisema wamekwenda mkoani huko kwa mambo mawili, kisasi na kuchukua pointi tatu. 


Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amesema wamejiandaa vizuri na wapo tayari kwa mchezo huo na kuchukua pointi tatu.


"Walitusumbua kweli, walitufunga mabao matatu, kwa sasa tupo vizuri, nawaambia Tabora United kwa niaba ya wachezaji wenzangu, walikuja kwetu, lakini sasa tupo kwao, pointi tatu tunazitaka, tumejipanga vizuri kulipiza kisasi," alisema Mwamnyeto.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu uliopigwa, Uwanja wa Azam Complex Novemba 7 mwaka jana, Dar es Salaam, Yanga ilikutana na kipigo cha kushtukiza cha mabao 3-1 dhidi Tabora United.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miloud Hamdi, amesema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kucheza na timu ambayo ilipata ushindi kwenye mchezo wa kwanza, hivyo watajitutuma, lakini wao wamejipanga kuonyesha kwamba ni timu kubwa.


"Yanga ni timu kubwa, tunakwenda kucheza mechi ngumu, timu hii ilipata ushindi mchezo uliopita, safari hii tumejipanga kuwapa furaha wanachama na mashabiki wa Yanga, nadhani watajitokeza kwa wingi kama kawaida yao kuwapa sapoti wachezaji kama ambavyo huwa wanafanya kwenye michezo yote," alisema kocha huyo.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet