pmbet

Wamarekani wawili wauawa na magenge yenye silaha nchini Haiti

Eric Buyanza

May 25, 2024
Share :

Raia wawili wa Marekani ni miongoni mwa wamishonari watatu waliopigwa risasi na kuuawa na watu wenye silaha kwenye mji mkuu wa Haiti, eneo ambalo kwa muda sasa limekuwa likikabiliwa hali mbaya ya usalama kutoka kwa magenge yenye silaha. 

Taarifa ya msemaji wa polisi nchini Haiti imesema wamishonari hao waliuawa baada ya watu wenye silaha kuvamia nyumba yao, kupora mali na kisha kuwaua.

Ikulu ya Marekani katika taarifa yake kuhusu mauaji hayo, imesisitizia mpango wa kuwatuma polisi wa Kenya nchini Haiti kuongoza kikosi cha polisi wa kimataifa kukabiliana na machafuko yanayoendelea.

Hivi karibuni Rais Biden wakati wa kikao na mwenzake wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya White House, walijadili kwa upana kuhusu suala hilo.

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa na mauaji hayo.

Rais wa Kenya William Ruto wakati wa ziara yake mjini Washington aliapa kwamba kikosi cha usalama cha nchi yake nchini Haiti kitafanya kila juhudi kuangamiza magenge hayo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet