Wameagana salama
Sisti Herman
March 11, 2024
Share :
Hatimaye vita ya kocha Jurgen Klopp na Pep Guardiola kwenye ligi kuu Uingereza imetamatika rasmi kwa sare baada klabu wanazofundisha, Liverpool na Man City kugawana alama kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa bao 1-1 na kushuhudiwa Pep akimuaga mshindani wake Klopp ambaye alitangaza mapema mwaka huu kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho Anfield.
Magoli ya timu hizo leo yamefungwa na John Stone kwa upande wa Man City akimalizia kona huku lile la Liverpool likifungwa na Alexis McAllister kwa mkwaju wa penalti.
Hadi sasa kwa ujumla, Pep na Klopp wamekutana mara 30, Klopp akishinda mara 12, Pep akishinda mara 11 na sare 7.