Wameishaa... Halland kurejea uwanjani leo
Joyce Shedrack
January 31, 2024
Share :
Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Halaand (23) raia wa Norway rasmi amerejea mazoezini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata, Kocha Mkuu wa klabu hiyo Pep Guardiola amethibitisha kuwa ataanza kumtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo ujao.
“Haaland amerejea baada ya kupata majeraha, tuna kikosi kamili tupo imara ni mchezaji muhimu kwetu ,hatuna majeruhi tena Manuel Akanji ameanza mazoezi na John Stones pia”amesema Guardiola
Haaland hajaonekana uwanjani tangu disemba 6 kwa sababu ya jeraha la mguu alilokuwa amelipata na amekosekana kwenye michezo kumi ya mashindano yote msimu huu.
Mshambuliaji huyo ameifungia timu yake magoli 19 katika michezo 22 aliyocheza msimu huu, atarejea leo uwanjani kucheza dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza (EPL).
Man City ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa wamekusanya alama 43 katika michezo 20 aliyocheza.