Wanafunzi 1,000 na walimu wao, wanajisaidia kwenye shule ya jirani
Eric Buyanza
February 22, 2024
Share :
Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood ameonesha kusikitishwa baada ya kubaini wanafunzi zaidi ya 1,000 pamoja na walimu wao katika shule ya msingi Mgulu wa Ndege, Manispaa ya Morogoro hawana vyoo na kulazimika kwenda kujisitiri katika shule jirani ya Mkundi.
Abood amejionea hali hiyo baada ya kufanya ziara ya kikazi kwenye Kata ya Mkundi na kupokelewa Diwani wa Kata hiyo, Seif Zahoro Chomoka pamoja na Diwani wa Viti Maalum, Grace Mkumbae, viongozi wa chama, viongozi wa serikali na wananchi.
Akiwa katika shule ya Msingi Mgulu wa Ndege, Mbunge hiyo amebaini kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa vyoo, hivyo ameamua kuwa atajenga choo cha walimu wa shule hiyo.
Licha ya kujenga choo cha walimu pia atachangia kiasi cha Sh milioni moja zitakaziotumia kulipa fundi atakayejenga vyumba vya madarasa vilivyotokana na nguvu za wananchi.
Kwa upande wa vyoo vya wanafuzi wa shule hiyo alimwomba Mkurugenzi wa Manispaa kusimamia ujenzi wake, licha ya kusema kuwa serikali itajenga vyoo vya wanafunzi na kazi hiyo itaanza mapema iwezekanavyo.