Wanafunzi 10,000 waliochaguliwa sekondari, hawajaripoti shule mpaka leo
Eric Buyanza
March 13, 2024
Share :
Wanafunzi zaidi ya sh 10,000 kati ya 56,827 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika Shule za Sekondari za Serikali mkoani Morogoro hawajaripoti shuleni hadi kufikia Februari 23, 2024.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Elimu Taaluma mkoa wa Morogoro, Hildegard Saganda wakati akiwa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa.
Taarifa imeeleza kuwa hadi kufikia Februari 23 idadi ya wanafunzi walioripoti na kusajiliwa shuleni hapo ilikuwa 46,775 sawa na asilimia 82 kati yao wavulana ni 22,203 na wasichana ni 24,572.
NIPASHE