Wanafunzi 20 wafariki katika ajali ya basi la shule
Eric Buyanza
July 17, 2026
Share :

Takriban wanafunzi 20 wamefariki dunia baada ya basi la shule ya King David Junior School ya jijini Kampala nchini Uganda kupata ajali usiku wa kuamkia leo wakati wakirejea kutokea kwenye ziara ya masomo katika kivutio cha Sipi Falls.
Kwa mujibu wa taarifa za awali za polisi, dereva alipoteza muelekeo wa basi kabla ya kugonga jiwe kubwa kando ya barabara na basi hilo kupinduka.
"Uchunguzi wa awali unaashiria kuwa basi lilipoteza mwelekeo kutokana na hitilafu ya kiufundi. Pia tumebaini kupitia ushahidi wa mashuhuda kuwa gari hilo lilisimama mara kadhaa kabla ya ajali kutokea," polisi walisema katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii.
Ajali hiyo imezua simanzi nchini Uganda, wakati familia za wanafunzi na viongozi wa shule wakisubiri taarifa rasmi kuhusu hatima ya waliokuwa ndani ya basi hilo.





