Wanafunzi UDSM wabuni vitambaa kwa kutumia chupa za plastiki
Eric Buyanza
May 31, 2024
Share :
Wanafunzi wabunifu kutoka Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam (UDSM) wametengeneza vitambaa vya kutengenezea nguo kwa kutumia chupa za plastiki.
Chupa hizo za plastiki huyeyushwa na kwenda kutengenezea nguo, ubunifu ambao umewavutia watu wengi kwenye maonyesho ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayofanyika jijini Tanga katika viwanja vya Popatlal.
Wanafunzi hao hutumia mashine kusaga chupa hizo za plastiki na kuwa vipamde vidogo vidogo vinavyochomwa na kugandamizwa na mashine maalum na kisha kutengeneza nyuzi zinazoweza kutumika kushona vitu mbalimbali.