pmbet

Wanafunzi wawafunga walimu kwenye mti na kuwatembezea bakora

Eric Buyanza

April 6, 2024
Share :

Wajua Mwezi August mwaka 2022 lilitokea tukio la ajabu nchini india ambalo liliacha simulizi kila kona ya dunia.

Katika tukio la kushangaza wanafunzi wa kiume wenye hasira wa shule ya sekondari iliyopo mjini Jharkhand nchini India, waliwafunga kwa kamba chini ya mti walimu wao wa hisabati na kuwatembezea bakora ikiwa kama njia ya kumaliza hasira zao baada ya kufeli somo hilo.

Inaelezwa kuwa wanafunzi hao waliamua kutekeleza adhabu hiyo kwa walimu kwasababu ya kutoridhishwa na maksi walizopewa kwenye mtihani wao wa hesabu.

Gazeti la India Times liliripoti kuwa wanafunzi 11 katika darasa lenye wanafunzi 32 walipata alama ya D, ambayo ni sawa na kufeli, jambo ambalo lilizua hasira kwa wanafunzi wote. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet