pmbet

Wanahabari wa Afrika msiige Uzushi Ulaya - Onana

Sisti Herman

January 16, 2024
Share :

Baada ya taarifa nyingi kusambaa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kipa wa Manchester United na timu ya Tifa ya Cameroon Andre Onana iliyohusisha safari yake kujiunga na timu ya Taifa iliypo nchini I vory Coast saa chache kabla ya mchezo wa kwanza wa  AFCON akitokea kwenye klabu ambayo ilikuwa na mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Totenham Hotspurs huku wengi wakitafsiri kama kukosa uzalendo kwa Taifa, hatimaye ameamua kufunguka mara baada ya mchezo wa timu yake ya Taifa.

 

"Ninayo mengi ya kuongea kwasasa ila nimechagua kukaa kimya kwa heshima ya Timu yangu ya Taifa na Mpira wetu wa Afrika.. ila kwa ufupi waandishi wa Kiafrika wanapaswa kuacha kufuata mkumbo wa Waandishi wa Ulaya kuhusu udhalilishaji wanaoufanya kwangu"

"Ukweli ambao waandishi wengi walikuwa hawaujui kuhusu mimi jana ni kwamba Kocha alishaniambia mapema nikichza mechi dhidi ya Spurs hatonipanga katika mchezo wa jana AFCON na nililiheshimu hilo kwasababu mwenye kipaji cha kukaa golini kwetu Cameroon sio mimi pekeyangu, wapo vijana kama Okoa na ndio nilitamani wapangwe katika mchezo ule endapo nikikosekana na ikawa hivyo.."

"Mtu unachukua picha nikiwa Koridoni naongea mambo ya mpira na wakongwe kadhaa wa soka la Afrika alafu unaweka mitandaoni na kusema nilikuwa nimekasirika kisa sijapangwa kwenye mchezo.. hii sio sawa lakini nishawazoea.. ninachojua mimi nipo kwaajili ya kulipambania Taifa langu la Cameroon na ndio walioniamini hayo mengine nishazoea." alimaliza Onana akiongea na  Canal Sports.

Maneno ya Golikipa wa Cameroon, André Onana kuhusu Taarifa za uongo anazopakaziwa Mtandaoni baada ya Mchezo wa Jana

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet