pmbet

Wanajeshi 200 wa Traore wauawa na waasi Burkina Faso

Sisti Herman

May 16, 2025
Share :

Kundi moja la wapiganaji linalofungamana na kundi la al-Qaeda, huko Afrika Magharibi limesema kuwa mashambulizi yake yamewaua wanajeshi 200 wa Burkina Faso katika kambi moja ya kijeshi nchini humo.

 



Al Jazeera imeripoti leo Ijumaa Mei 16, 2025, kuwa kundi hilo maarufu kama Jama'a Nusrat ul-Islam wa al-Muslimin, (JNIM) limefanya mashambulizi hayo kwa nyakati tofauti wiki hii.

Awali jana, kundi JNIM lenye ushirika na kundi la Al-Qaeda, lilisema kwamba limewauwa wanajeshi 60 na idadi hiyo imeongeza na kufikia takriban 200.

Hata hivyo, Al Jazeera haikuthibitisha taarifa ya kundi hilo. Mamlaka za Burkina Faso zilipotafutwa kuzungumzia madai hayo hazikujibu chochote.

Ingawa hakujatolewa taarifa rasmi na Serikali, lakini wakazi watatu wa mji wa Kaskazini wa Djibo uliovamiwa, wameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa wanajeshi na raia wa Burkina Faso wameuawa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet