pmbet

Wanajeshi 25 wa Kongo wahukumiwa kifo kwa 'kumkimbia adui' wakati wa mapambano

Eric Buyanza

July 4, 2024
Share :

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Wanajeshi 25 wanaotuhumiwa "Kumkimbia adui" wakati wa mapambano na waasi wa M23 walihukumiwa kifo jana (Jumatano), taarifa kutoka kwa mawakili wao ilisema.

Wanajeshi hao walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi ya Butembo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, wakikabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo kukimbia adui, kuharibu silaha za kivita, kukiuka amri na wizi, Jules Muvweko, mmoja wa mawakili wa utetezi aliliambia shirika la habari la AFP.

Tangu wiki iliyopita, M23 wamechukua miji kadhaa nchini humo ukiwemo mji wa kimkakati wa Kanyabayonga, ambao unaonekana kama lango la vituo vikuu vya kibiashara vya Butembo na Beni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet