pmbet

Wanajeshi 54 wa DRC wanashtakiwa kwa kutoroka vitani!

Eric Buyanza

October 31, 2026
Share :

Mahakama ya Kijeshi ya mkoa wa Goma, imeanza kuwashtaki wanajeshi 54 kutoka Kikosi cha 3415 cha Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC). Askari hao wanakabiliwa na msururu wa mashtaka mazito ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kuwakimbia waasi wakati wa mapambano.

 

Msemaji wa Jeshi katika Kanda ya 34 ya Kijeshi amethibitisha kuwa wanajeshi hao walikamatwa mnamo Oktoba 20 katika kijiji cha Ngora, wilayani Walikale na kesi yao ilianza kusikilizwa rasmi Jumatatu, Oktoba 26, 2026.

 

Kulingana na nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, baadhi ya wanajeshi wanakabiliwa na mashtaka matano mazito yanayohusiana na oparesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa (FRN) katika maeneo ya Masisi na Walikale.

 

Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa utovu mkubwa wa nidhamu na kukiuka viapo vyao vya kazi. Mashtaka yanayowakabili ni pamoja na uoga mbele ya adui na kutoroka jeshini, ambapo wanadaiwa kukimbia na kuacha vituo vyao vya kazi wakati wa mapambano bila kibali wakati wa mashambulizi ya waasi.

 

Aidha, wanakabiliwa na shtaka la mauaji kufuatia vifo vilivyotokea wakati wa vurugu hizo, pamoja na matumizi mabaya ya zana za kivita kwa kutumia ovyo silaha na risasi walizokabidhiwa.

 

Mbali na hayo, wanajeshi hao wanatuhumiwa kukataa kutii amri kwa kukaidi maagizo halali ya makamanda wao wa ngazi za juu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet