pmbet

Wanajeshi wa Israeli waonekana karibu na mpaka wa Lebanon

Eric Buyanza

March 31, 2026
Share :

Wanajeshi wa Israeli wameonekana karibu na mpaka wa nchi jirani ya Lebanon, hatua inayojiri wakati huu Israeli ikiripotiwa kuendelea kurusha makombora nchini Lebanon.

 

Jeshi la Israel linasema, mashambulio nchini Lebanon yataendelea katika kile linasema ni juhudi zake na kupambana na wapiganaji wa Hezbollah.

 

Lebanon ilitumbukia kwenye mzozo unaoendelea mashariki ya kati Machi 2 baada ya wapiganaji wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran kurusha makombora kuelekea Israeli.

 

Tangu wakati huo, Israeli imewaagiza wakaazi wa kusini mwa Lebanon kuondoka, ikitekeleza mashambulio na oparesheni kwenye eneo hilo katika kile inasema ni juhudi zake na kupambana na wapiganaji wa Hezbollah.
 

Zaidi ya watu 1,200 wameuawa kwenye mashambulio nchini Lebanon kwa mujibu wa serikali nchini humo, wakiwemo watoto 120 na wanawake 80 wakiwemo wahudumu wa afya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet