pmbet

Wanajeshi wahukumiwa Burundi kisa kugoma kwenda vitani

Sisti Herman

June 26, 2024
Share :

Wanajeshi 274 wa Burundi waliogoma kwenda kupigana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamehukumiwa vifungo kati ya miaka 20 na 30 baada ya kukutwa na hatia ya kukaidi amri ya Kijeshi.

Mahakama ya kijeshi imewahukumu Wanajeshi hao ambapo wao walisema kuwa wakati wanapelekwa nchini Jamhuri ya Kidemlokrasia ya Congo hawakujulishwa ni kipi wanakwenda kufanya.

Wanajeshi hao wamedai kukiukwa kwa haki zao za binadamu huku wakisema kuwa wanakwenda kukataa rufaa kuhusiana na hukumu hiyo.

Wakiwa 274 wamefungiwa katika Gereza mbali mbali ikiwemo Ngozi, Rumonge,Cankuzo,Ruyigi,Bururi na mkoani Rutana ambapo hukumu ilipotolewa.

Kesi ya Askari hao ilimaliza siku 28 baada ya kuanza kusikilizwa tarehe 22 za mwezi Mei hadi Juni 18 mwaka huu.

Wote walikamatwa mwishoni mwa mwaka uliopita hadi mwezi Aprili mwaka huu walio wengi wakiwa walitoka Mashariki mwa DRC, wakiwemo Makanali, Meja, Kapteni wakisema kuwa walifuata sheria za kijeshi kukataa kupigana na waasi wa M23.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet