pmbet

"Wanajeshi wangu wanapitia wakati mgumu kwenye uwanja wa vita" - Zelensky

Eric Buyanza

July 27, 2024
Share :

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kuwa wanajeshi wake wanakabiliwa na wakati mgumu katika uwanja wa mapambano kutokana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo. 
 

Katika hotuba yake kwa taifa kwa njia ya video, Zelensky ameeleza kuwa hivi karibuni maeneo karibu na mji wa Pokrovsk katika mkoa wa Donetsk yamelengwa na vikosi vya Urusi.
 

Kiongozi huyo ametoa mwito wa kuimarisha ulinzi zaidi katika maeneo hayo.
 

Kauli ya Zelensky ameitoa baada ya idara ya ujasusi ya Ukraine kueleza mapema leo kuwa vikosi vya Urusi vimeelekeza nguvu zaidi katika eneo la Donbass mashariki mwa nchi hiyo na lenye utajiri wa makaa ya mawe. 
DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet