Wanajeshi wawili wa China wavujisha nyaraka za siri kwa Wamarekani.
Sisti Herman
June 16, 2024
Share :
Wizara ya Usalama wa Taifa imesema Maafisa Wawili wa Jeshi la China (Guo na Li) waliotakiwa kuziharibu nyaraka za siri takriban 200 waliziuza katika Kiwanda cha kuchakata taka kwa chini ya Dola 4 za Marekani
Tukio hilo limebainika baada ya Mstaafu mmoja aliyetajwa kwa jina la Zhang, ambaye hununua Majarida na Vitabu kuhusu mambo ya Jeshi kama Hobby, kununua nyaraka 8, miongoni mwa Nyaraka 200 zilizokuwa katika Mifuko Miwili katika Kiwanda cha Kuchakata taka
Imeelezwa baada ya kusoma baadhi ya Nyaraka hizo Zhang alitoa taarifa kwa Mamlaka kupitia namba ya Mtandaoni, ambapo Maafisa wa Jeshi walifika nyumbani kwake mara moja na kuzichukua nyaraka hizo
Hata hivyo, Wizara imesema tukio hilo halijasababisha uvujaji mkubwa wa taarifa za Kijasusi na Guo na Li, pamoja na yeyote aliyehusika wameshughulikiwa kwa Mujibu wa Sheria za Nchi