pmbet

Wanamuziki wa dansi hawaitendei haki mitandao ya kijamii - Asha Baraka

Eric Buyanza

June 6, 2025
Share :

Mwenyekiti wa Bendi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka (Iron Lady), amewapa makavu wanamuziki wa dansi kuhusu kutumia mitandao ya kijamii, kwani imechangia kurudisha muziki huo nyuma ukilinganisha na wenzao wa Bongo Fleva.

“Wanamuziki wa dansi asilimia kubwa hawaitendei haki mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusapoti huu muziki wa dansi, ukweli katika hili suala wanahitaji elimu sana ili waweze kupata ufahamu wa faida ya mitandao ya kijamii kwa matumizi ya kazi zao.

Yaani utakuta mtu hata kuposti kazi zake kwenye mitandao haposti na wengine hadi sasa wala hawana akaunti za mitandao, inatakiwa watambue hakuna kazi isiyoonekana mfano mimi kiongozi wa Twanga Pepeta, Chaz Baba haposti chochote katika mitandao, yaani hii nasema kwa ujumla pia wanamuziki wa dansi wanajiangusha wenyewe.

“Hali ni tofauti na wasanii wa Bongofleva na miondoko mingine, wanachangamkia mitandao sababu wale wanafanya kazi binafsi wanajiajiri wenyewe, lakini muziki wa dansi mfano Twanga Pepeta watamtegemea Asha Baraka au watategemea wataonekana katika akaunti za bendi, lakini hata hawajui kama ipo siku mtu atatoka Twanga Pepeta.

“Leo nikiongozana na mwanamuziki wa dansi barabarani utashangaa naitwa mimi, sasa unajiuliza mimi naimba? Lakini hii inatokana na kazi yangu ya kufanya jitihada, watu wanifahamu” anasema Asha.

MWANASPOTI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet