Wananchi haooo kileleni, Wawapiga Namungo kwao
Sisti Herman
March 8, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imeshinda mchezo ligi kuu ugenini dhidi ya klabu ya Namungo kwa mabao 3-1 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi na kurejea juu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Mudathir Yahya, Clement Mzize na Stephanie Aziz Ki huku bao pekee la Namungo likiwa la kujifunga la beki wa Yanga Ibrahim Bacca.