pmbet

Wananchi jiandaeni kufurahi, Dodoma Jiji hachomoki

Joyce Shedrack

February 5, 2024
Share :

Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Februari 5, 2024 kwa mechi moja ambapo Wananchi, Young Africans SC watakuwa na kibarua dhidi ya Wakulima wa zabibu, Dodoma Jiji FC katika dimba la Azam Complex, Chamazi saa 1:00 jioni.

 

Wananchi wanashuka dimbani katika mchezo wao wa 13 kwenye ligi kuu msimu huu wakiwa tayari wameshacheza michezo 12 na kukusanya alama 31, Dodoma Jiji wapo nafasi 7 kwenye msimamo wa Ligi  wameshashuka dimbani mara 13 na kukusanya alama 18.

 

Meneja wa klabu ya Yanga, Walter Harrison amethibitisha kuwa kikosi kipo katika hali nzuri isipokuwa 'Babu Kaju' ambaye ameumia bega.
 

Amesema Sure Boy ambaye kwa mujibu wa Daktari mfupa mmoja wa bega ulihama anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na baada ya wiki mbili atarejea kwenye mazoezi.

 

Tangu wapande daraja, Dodoma Jiji wameifuata Yanga Dar es Salaam mara tatu na wamepoteza mara zote huku wakiruhuru magoli 11 na kufunga mabao mawili pekee.

 

Rekodi za michezo ya timu hizi mbili zilipokutana kwenye ligi kuu soka Tanzania bara zinaonyesha matokeo ya afadhali Dodoma Jiji aliyowahi kuyapata dhidi ya Yanga ni sare ya bila kufungana aliyoipata july 18 mwaka 2021 Dodoma Jiji akiwa mwenyeji wa mchezo huo.
 

MECHI TANO ZA MWISHO YANGA VS DODOMA JIJI
 

13 May 2023 NBC Premier League

FT Young Africans 4 – 2 Dodoma Jiji
 

22 November 2022 NBC Premier League

FT Dodoma Jiji 0 – 2 Young Africans
 

15 May 2022 NBC Premier League

FT Dodoma Jiji 0 – 2 Young Africans
 

31 December 2021 NBC Premier League

FT Young Africans 4 – 0 Dodoma Jiji18 
 

July 2021 NBC Premier League

FT Dodoma Jiji 0 – 0 Young Africans
 

Dodoma Jiji wanakwenda kuchuana na Yanga wakiwa na kocha mpya Francis Baraza aliyewahikuzinoa Kagera Sugar na Biashara United kabla ya kurejea kwao Kenya.

 

Leo ni vita kati ya  kocha Francis Baraza dhidi ya master Miguel Gamondi nani kuibuka mshindi ?

 

  

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet