Wananchi kumshuhudia Shalulile kwa mara ya kwanza Agosti 9.
Joyce Shedrack
July 28, 2026
Share :
Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kufanya kilele cha siku ya Wananchi Agosti 9 kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Katika Tamasha hilo Wananchi wanatarajia kutambulishwa wachezaji wao wapya pamoja na kuwashuhudia kwa mara ya kwanza nyota wao wapya waliosajiliwa katika dirisha kubwa la usajili.
“Tamasha la Wiki ya Mwananchi la msimu huu limeongezeka thamani kwa sajili tulizofanya maana mashabiki kwa mara ya kwanza watapata nafasi ya kuwashuhudia wachezaji wetu wakiwa wanacheza klabu ya Yanga sc kwenye uwanja wa uhuru siku ya tarehe 09” Ally Kamwe





