Wananchi kuna habari zenu huku
Sisti Herman
March 25, 2024
Share :
Kupitia ukurasa wa instagram wa klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika kusini dakika chache zilizopita kwa lugha ya kiswahili wamechapisha "Habari Masandawana Muwe na wiki njema!".
Masandawana kama wanavyojulikana, ni wapinzani wa klabu ya Yanga kwenye robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika na mchezo wa kwanza utachezwa mwishoni mwa juma hili kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es salaam, Hivyo ni wazi kuwa salaam hizo zimewalenga mashabiki zao ambao wapo Tanzania.