Wananchi kuzisaka alama tatu leo dhidi ya Singida BS.
Joyce Shedrack
May 22, 2026
Share :
Klabu ya Yanga inatarajia kushuka uwanjani leo majira ya saa 10 jioni kwenye mchezo wa ligi kuu siku ya leo dhidi ya Singida Black Stars kwenye uwanja wa KMC Complex.

Wananchi wanasaka alama 3 kwenye mchezo huo ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya siku ya jana mtani wao kushinda mchezo wao na kuwa kinara kwa alama 55 nyuma ya Yanga mwenye alama 54 huku akiwa na mchezo mmoja mkononi.
Singida Black Stars nao wanahitaji alama tatu ili kujiweka pazuri kwenye kupamabania nafasi 4 za ligi na kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.
Nani atavuna alama tatu leo?.





