Wananchi waachwe wajiamulie mambo yanayohusu maendeleo yao - Kinana
Eric Buyanza
January 2, 2024
Share :
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulurhman Kinana amesema ipo haja ya kutoa fursa zaidi kwa wananchi kujiamulia mambo yanayohusu maendeleo yao.
Kinana ameyasema hayo jana Januari 1, 2024 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM na wanachi wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Amesema huenda haifanyiki sawa kutowapa wananchi fursa kubwa ya kuamua mambo yanayohusu maendeleo yao, jambo ambalo linasababisha kutofikia ufumbuzi wa baadhi ya changamoto katika vitongoni, vijiji au mitaa.
“Kiongozi unaweza ukaenda mahali na fikra zako mwenyewe ukifikiri shida ya watu ni shule, ni maji kumbe shida yao ni jambo jingine kabisa, hivyo ni lazima tuwashirikishe wananchi katika mambo yanayohusu maendeleo yao,” amesisitiza.
TSN