pmbet

Wananchi wakumbushwa madhara ya unywaji wa pombe kupita kiasi

Eric Buyanza

February 11, 2026
Share :

Wananchi wa Kata ya Chitete Wilaya ya Momba Mkoani Songwe wametakiwa kuacha na kuepuka unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na kuzingatia sheria na taratibu zinazohusu uendeshaji wa vilabu vya pombe, ikiwemo kufungua na kufunga kwa muda.

 

Akizungumza na wananchi hao tarehe 8 Februari 2026 wakati akiongea nao maeneo ya Vilabuni katika kata hiyo, Polisi Kata wa Chitete, Mkaguzi wa Polisi Makubi Lagae, alisema kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wamiliki wa vilabu na wauzaji wa pombe watakaokiuka muda wa kufungua na kufunga vilabu kama unavyoelekezwa.

 

Mkaguzi Chitete aliwaambia wananchi kuacha kunywa pombe kwa kupitiliza kwani kunasababisha matatizo ya afya,kukosa muda wa kujitafutia liziki na wakati mwingine unachangia migogoro isiyoyalazima katika jamii.

 

Katika kuhitimisha, Mkaguzi Makubi aliwahimiza wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za ukiukwaji wa sheria na viashiria vya uhalifu kwa wakati, huku akisisitiza kuwa usalama na ustawi wa jamii ni jukumu la kila mwananchi.

 

@polisi.tanzania

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet