"Wananchi wengi wa tabora hawajui kusoma na kuandika" - Mtakwimu
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
Mkoa wa Tabora umetajwa kuwa nyuma Kitaifa kwa watu wanaojua kusoma na kuandika ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.
Taarifa hiyo imetolewa Machi 14, 2024 jijini Dar es Salaam na Mtakwimu Mwandamizi Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Omary Mdaka, wakati akiwasilisha mada katika Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana Usambazaji na Uhamasishaji wa Matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022.
Mdaka amesema kuwa, katika zoezi hilo la ukusanyaji takwimu mbali mbali, pia imebainika kuwa, kwa upande wa elimu, Mkoa wa Tabora ndio upo nyuma kwa idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika kwa kiwango cha asilimia 68.0 ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini.
“Imebainika wananchi wengi wa Tabora hawajui kusoma na kuandika na hii itasaidia kufanya utafiti zaidi kujua sababu hasa zinazopelekea mkoa huo kuwa nyuma kwa kiasi hiki,” amesema Mdaka.
GAZETI/MTANZANIA