pmbet

Wananchi zaidi ya 500 Mkoani Arusha hatarini kufia usingizini.

Joyce Shedrack

July 1, 2024
Share :

Watu takribani 600 wamegundulika kuwa na matatizo mbalimbali ya moyo kati ya watu 1500 waliohudumiwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho kikwete kwenye kambi maalum ya matibabu ya kibingwa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Peter Kisenge ametoa Takwimu hizo wakati alipokuwa akitoa tathimini ya huduma za taasisi hiyo wakati wa kambi hiyo ya matibabu ya siku nane inayotarajiwa kumalizika siku ya leo.

Daktari Kisenge amesema miongoni mwa magonjwa ya moyo yenye kuwasumbua wananchi wengi wa Arusha ni pamoja na moyo kuwa dhaifu kwa kushindwa kufanya kazi zake kikamilifu suala ambalo limekuwa likisababisha vifo vya ghafla wakati mtu akiwa usingizini.

Aidha daktari huyo amesema jumla ya watoto 150 walipimwa na kupatiwa matibabu na Taasisi hiyo ambapo kati yao watoto 53 wamegundulika kuwa na matatizo ya valvu kwenye moyo na hivyo kuhitaji upasuaji mkubwa unaotakiwa kufanyika Jijini Dar Es salaam.

Awali, kambi hiyo ya matibabu ilipaswa kumalizika siku ya jana lakini kutokana na uhitaji wa Wananchi na matibabu kwa baadhi ya watu kushindwa kukamilika Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alitangaza kuongeza siku moja kwa ajili ya kumalizia matibabu kwa baadhi ya watu waliokuwa wamesalia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet