pmbet

Wanandoa waliofuga paka 159 wahukumiwa kifungo na marufuku ya kufuga tena

Eric Buyanza

April 4, 2024
Share :

Huko nchini Ufaransa wanandoa wawili wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kufuga wanyama katika mazingira ya ukatili.
 
Wanandoa hao, kutoka mjini Nice, walikuwa wamefuga paka 159 na mbwa saba katika nyumba yao ya ghorofa wanayoishi.
 
Wanyama hao waligunduliwa wakiwa wanaishi katika mazingira machafu, wakiwa wamepungukiwa maji....wana utapiamlo na magonjwa mengine yatokanayo na uchafu.

Kwenye hukumu iliyotolewa, wanandoa hao pia wamepigwa marufuku ya kudumu ya kufuga tena wanyama.
 
Mahakama iliwaamuru kulipa €150,000 sawa na (shilingi milioni 425 za kibongo) kwa mashirika ya haki za wanyama.
 
Mwaka jana, polisi walivamia nyumba na kukuta makumi ya paka katika kila eneo la nyumba hiyo.
 
Mamlaka ziliripoti uwepo wa kinyesi cha wanyama kila mahali kwenye nyumba hiyo huku wakisema baadhi ya paka na mbwa hao walikufa kwa sababu ya kuwa na afya mbaya. Pia iligundulika miili ya paka wawili na mbwa wawili ikiwa bafuni.
 
Katika hali ya kushangaza, wanandoa hao waliiambia mahakama kwamba wanyama hao walikuwa "kipenzi cha maisha yao" lakini walikuwa "wamezidiwa na malezi". 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet