Wanandoa waliopishana miaka 37 wanatarajia mtoto wao wa kwanza
Eric Buyanza
May 15, 2024
Share :
Stori iliyozua minong'ono mingi kwenye mitandao ya kijamii wiki hii ni ile ya mwanamke wa miaka 63 na mume wake mwenye umri wa miaka 26 kutarajia kupata mtoto wao wa kwanza pamoja.
Cheryl McGregor na Quran McCain, kutoka Georgia, nchini Marekani, wamejikusanyia mamilioni ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuanika mahusiano yao hadharani.
Katika video ya hivi majuzi waliyoitupia TIKTOK, McGregor aliandika: "Hatimaye inakuwa, tunaanzisha familia yetu."