pmbet

Wananichukia kwa sababu baba yangu ni tajiri - Davido

Eric Buyanza

May 14, 2025
Share :

Staa wa muziki wa Afrobeats kutoka nchini Nigeria, David Adeleke (Davido) amesema yeye ndiye mtu maarufu anayekosolewa zaidi nchini Nigeria kwa sababu tu anatokea kwenye familia ya kitajiri.

Davido anasema unyanyapaa wa "mtoto wa kitajiri" ungeathiri sana kazi zake kama siku za mwanzo asingeficha ukweli kuhusu maisha yake.

“Mimi ndiye msanii ninayekosolewa zaidi nchini Nigeria, watu hawakujua kuwa baba yangu ni tajiri na walipokuja kujua tayari nilikuwa nina ngoma tatu hewani zinazovuma”

“Baada ya muda, watu walianza kunichukia kwa sababu ya utajiri wa baba yangu, lakini ninaendelea kufanya muziki mzuri na unaendelea kufanikiwa.

"Inatokea kwa kila mtu, ukishakuwa mkubwa katika jambo lolote, utakosolewa" alimalizia Davido.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet