pmbet

Wanaobeba watoto kwenye bodaboda kukiona

Eric Buyanza

January 5, 2024
Share :

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Ramadhan Ng’anzi ametangaza kuanzia wiki ijayo wakati shule zitakapokuwa zikifunguliwa, dereva wa bodaboda atakayeonekana amebeba mtoto chini ya miaka tisa, atachukuliwa hatua za kisheria yeye na mzazi."
 

Kamanda Ng’azi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na chombo kimoja cha Habari, ambapo pia amesema kwa magari maalumu ya kubebea wanafunzi ambayo hayajafanyiwa ukaguzi hadi kufikia wiki ijayo wakati shule zinafunguliwa, yatafungiwa.
 

“Wazazi wanaotumia bodaboda kuwapeleka na kuwarudisha shule watoto wao, wahakikishe watoto hao wana umri wa miaka tisa na kuendelea kama ana umri chini ya huo ampandishe bajaji.
 

Akipanda bajaji ahakikishe hawajazani, na tukikuta mtoto wa chini ya miaka tisa amepakiwa kwenye bodaboda, mzazi na dereva wa bodaboda watachukuliwa hatua za kisheria,” amesema Kamanda Ng’anzi.
 

“Magari yatakayobainika yamebeba wanafunzi bila kufanyiwa ukaguzi tutamshtaki mmiliki wa shule na magari hayo pamoja na kuyazuia kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufutiwa leseni yake ya kubeba wanafunzi,” amefafanua.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet