pmbet

Wanaohifadhi pesa sehemu za siri kuburuzwa mahakamani

Eric Buyanza

June 7, 2024
Share :

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya watu ambao wamekuwa na tabia ya kuhifadhi fedha kwenye maziwa, soksi, chini ya magunia na kufunga fundo kwenye kanga, ikisisitiza kunafedhehesha fedha ya Tanzania. 

Pia imepiga marufuku fedha kuhifadhiwa sehemu za siri pamoja na kutengenezwa mataji kwenye sherehe, atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa vitendo hivyo ni kosa la jinai.

Baadhi ya hatua zitakazochukuliwa ni wahusika kufikishwa mahakamani kwa kuwa noti na sarafu ni sehemu ya nyara za serikali. Zinapaswa kuthaminiwa.
Meneja Idara ya Uendeshaji wa BoT Tawi la Dodoma, Nalasco Maluli, alitoa angalizo hilo juzi jijini wakati akiwasilisha mada katika  mafunzo ya waandishi wa habari kutoka mikoa saba ya Tanzania Bara; Iringa, Morogoro, Dodoma, Singida, Kigoma,Tabora na Njombe.

Maluli alisema fedha hizo za Tanzania ni sehemu ya tunu za taifa, hivyo zinapaswa kuheshimiwa kama ilivyo Bendera ya Taifa na kuanzia sasa yeyote atakayebainika kufedhehesha atachukuliwa hatua za kisheria.

"Tunaomba mkaelimishe wananchi kwa kutumia vyombo vyenu kuwa fedha ya Tanzania ni tunu ya taifa, hawatakiwi kuchana wala kuharibu kwani sheria imeshapitishwa tayari, atakayebainika tunamfikisha mahakamani," alisema Maluli.

Alisema fedha hizo za Tanzania zinatengenezwa kwa gharama kubwa kwa kutumia fedha za kigeni, hivyo zinapotunzwa vizuri zitatumika kwa muda mrefu na kupunguza gharama ya kutengeneza fedha nyingine kwa kutumia fedha za kigeni.

Meneja Msaidizi Sarafu BoT Dodoma, Matilda Luunga, alisema umefika wakati kwa wafanyabiashara wa vitu mbalimbali kuacha kuweka fedha chini ya magunia kwa kuwa unyevunyevu unasababisha kuharibu fedha.
"Kuna watu wa buchani, wanauza nyama na kuacha damu zinatiririka kwenye fedha na kusababisha zisikae kwa muda mrefu, tunataka wawe makini kwani tukiwabaini tu sisi tutawapeleka mahakamani," alisema Matilda.

Alisema ipo pia tabia imezuka kwenye harusi na sherehe mbalimbali wamekuwa wakitengeneza mataji ya fedha, akiwataka kuacha tabia hiyo. Noti haipaswi kutengenezwa taji kwa kuwa ni tunu ya taifa kama ilivyo Bendera ya Taifa.
NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet