Wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsia Moja kufungwa Jela Miaka 30
Sisti Herman
May 7, 2024
Share :
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi maalumu imesema jana Bungeni kuwa ni kosa la jinai kujihusisha na Mapenzi ya jinsia moja ambapo Naibu Waziri wa wiza hiyo Mwanaidi Khamis akitaja adhabu stahiki. “Kitendo cha kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni kosa la jinai […] mtu yeyote ambaye atapatikana na hatia ya kosa hilo ataadhibiwa kifungo cha miaka 30, ikithibitika na mtendewa aliridhia kufanyiwa kitendo hicho basi atahusika na kosa hilo hilo.” - Mwanaidi Khamis, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum