Wanariadha wa Afrika matatani kwa kupunguza mwendo ili mchina ashinde
Eric Buyanza
April 16, 2024
Share :
Waandaaji wa mbio za Nusu Marathon za Beijing nchini China, wametangaza kuwa wanachunguza madai ya wanariadha watatu kutoka Afrika waliomruhusu kimakusudi mwanariadha wa China, He Jie kushinda mbio hizo.
Picha za video zinawaonesha wanariadha Robert Keter (Kenya) Willy Mnangat (Kenya) na Dejene Hailu (Ethiopia) waliokuwa wakielekea kwenye mstari wa kumaliza...wakipunguza mwendo wakimuacha mwanariadha, He Jie (China) aliyekuwa nyuma yao akiwapita na kumaliza.
AFP