pmbet

Wanasayansi wagundua sukari anga za mbali

Eric Buyanza

July 17, 2026
Share :

Wanasayansi wamegundua sukari halisi katika anga za mbali (interstellar space), kwenye wingu kubwa la vumbi na gesi karibu na katikati ya kundi la nyota la Milky Way.
 

Watafiti kutoka Kituo cha Astrobiolojia cha Uhispania walitumia darubini kubwa za redio nchini Uhispania kugundua sukari hiyo katika wingu la molekuli linalojulikana kama G+0.693-0.027

 

Sukari iliyogunduliwa inaitwa erythrulose. Hapa duniani, sukari hii hupatikana kwa kiwango kidogo kwenye matunda aina ya 'Raspberries'.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa sukari halisi yenye kaboni nne kugunduliwa ikielea yenyewe kwenye anga za mbali, nje ya mfumo wetu wa jua. Huko nyuma, chembechembe za sukari kama ribose ziliwahi kupatikana tu ndani ya miamba ya vimondo.

 

Ugunduzi huu unathibitisha kuwa viungo vikuu vinavyounda mifumo ya uhai (kama DNA na RNA) vinaweza kutengenezwa angani hata kabla ya sayari na nyota kuanza kuumbwa. Wanasayansi wanakadiria kuwa mamilioni ya tani ya sukari hii yalishushwa duniani kupitia migongano ya asteroidi miaka bilioni 4 iliyopita, na kusaidia kuchochea mwanzo wa uhai.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet