Wanaume fuateni Sunna zote, siyo kuoa wake wengi tu
Sisti Herman
January 2, 2024
Share :
Mfalme wa Singeli kama anavyojiita mwanamuziki wa singeli nchini Dulla Makabila kupitia mtandao wake wa kijamii amewatolea povu wanaume wanaooa wake wengi kwa kigezo cha kukimbilia dini.
“Wanaume wenzangu kama kweli tunataka kufuata sunna za Mtume basi tuzifuate zote na siyo moja ya kuoa mke zaidi ya mmoja na mengine tunaachana nayo” ulieleza sehemu ya ujumbe wa Dulla kupitia insta story yake.