Wanaume hatujaumbwa kuwa na mpenzi mmoja -Akon
Eric Buyanza
April 28, 2026
Share :

Mwanamuziki mwenye asili ya Senegal anayefanyia shughuli zake nchini Marekani, Akon, amezua mjadala mtandaoni baada kunukuliwa akisema mwanaume kuwa na wapenzi wengi sio kitu cha ajabu kwa kuwa hilo ni jambo la asili.
Akiongea na The Shade Room alisema;
"Wanaume hawajaumbwa kuwa na mpenzi mmoja, sio kosa letu, ni asili tu” anasema Akon.
"Ninaamini katika mitala (ndoa ya wake wengi) lakini kwa wanaume tu, wanawake hawaruhusiwi kuwa na mume zaidi ya mmoja kwa sababu wanawake wanaweza kuzaa mtoto mmoja tu kwa mwaka, lakini mwanamume anaweza kuzaa watoto elfu moja kwa mwaka.Tunazalisha kwa kuwa Mungu ametuumba tuwe hivyo....Kuna sababu ya hilo." alimalizia Akon





