"Wanaume hawasamehi usaliti, akikusamehe atakuadhibu maisha yako yote" - Jimoh
Eric Buyanza
February 23, 2024
Share :
Kupitia ukurasa wake wa Instagram muigizaji wa kinigeria Seun Jimoh amefikisha ujumbe kwa wanawake akiwaonya kutothubutu kusema ukweli (kufunguka) kama amewahi kuteleza na kumsaliti mpenzi wake akiamini atasamehewa.....kwasababu wanaume huwa hasamehi usaliti.
Jimoh anasema kwa usalama na kulinda penzi ni bora kwa wanawake wakaficha makosa yao.....
"Mpendwa ikiwa utachepuka, usi-confess (usikiri) kamwe! iweke kati yako na Mungu wako"
"Wanaume hawasamehi usaliti na ikiwa watakusamehe, watakuadhibu kwa maisha yako yote." alimalizia.