Wanaume Kenya wanaogopa kunitokea - Victoria Kimani
Eric Buyanza
July 11, 2025
Share :
Mwanamuziki wa Kenya, Victoria Kimani ameweka wazi kuwa hajawahi 'kutongozwa' na wanaume wa Kenya huku akisema wanaothubutu kufanya hivyo ni wale wenye asili ya kigeni.
Victoria aliyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano ya kipindi cha 'Box Pod'
"Sitongozwi Kenya. Hakuna mtu anayenikaribia, isipokuwa wale ambao sio wa hapa".
"Ni hawajiamini au wanadhani kwamba nitawakataa au hawajui jinsi ya [kunitokea]. Ni kama vile hawana mbinu" alisema.
Kwa mujibu wa Victoria, wanaume wanahitaji tu kujiamini, kunukia vizuri na kujifunza njia sahihi za kuwatokea wanawake kwasababu wakati mwingine hutumia lugha zisizofaa ambazo hufanya wanawake kuwakataa.