Wanaume wa Nigeria wanajua kutunza wanawake wao - Ayra
Eric Buyanza
March 13, 2026
Share :

Mwanamuziki wa miondoko ya Afrobeats kutoka Nigeria, Ayra Starr ameelezea sifa na kupendezwa na wanaume wa nchini kwake.
Akizungumza hivi karibuni kwenye kipindi cha 'Way Up with Angela Yee', Starr alisema wanaume wa Nigeria ni kama wanaume wa New York, wanasaidia wenza wao na wanajiamini sana.
Lakini hata hivyo, aliendelea kuonyesha mashaka kuhusu wanaume hao akisisitiza kwamba “wanaume ni wanaume tu.”
"Wanaume wa Nigeria wanapenda kutunza wanawake wao na wanajiamini sana, kwa hivyo naweza kusema ni sawa na wanaume wa New York. Lakini unajua tena....mwanaume bado anabaki kuwa mwanaume. Ni jambo la ulimwengu wote."





