Wanawake ni wasaliti kwenye mapenzi kuliko wanaume - Iyanya
Eric Buyanza
December 26, 2023
Share :
Kutoka Nigeria staa wa muziki Iyanya amefunguka ya moyoni kwanini anaamini wanawake ni wasaliti zaidi kwenye mahusiano kuliko wanaume.
Iyanya anasema kinachomfanya aamini hivyo ni kwasababu asilimia 99 ya marafiki zake hawajaoa mpaka sasa.....na wala hawana mpango huo kutokana na woga kwa sababu mademu zao (ma-Ex) walioachana nao waliwasaliti kimapenzi na wanaume wengine.
Kwa upande wake yeye anasema hawezi hata siku moja kumsaliti mpenzi wake kwa sababu anakuwa 'focused' sana anapokuwa katika mapenzi.
Mwanamuziki huyo pia alisema hawezi kumsamehe mpenzi wake pindi anapobaini amemsaliti.