Wanawake songwe wataja sababu ya kuziogopa kondom
Eric Buyanza
January 31, 2024
Share :
Huko Wilayani Ileje Mkoani Songwe, wataalam wa Afya wameombwa kuanza kutoa elimu ya matumizi ya kondom za kike ili kukabiliana na magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukwimwi.
Hayo yamekuja baada ya kuibuka kwa hoja za wanawake wilayani humo, ya kwamba wanaogopa kuzitumia kondomu hizo kutokana na ukubwa wake. Diwani wa Kata ya Itale, Fahari Mwampashi amesema watumiaji wa kondomu hizo wanasema ni kubwa ukilinganisha na maumbile yao na wametaka zipunguzwe.
“Wanawake wanaogopa kuvaa hizo kondomu wakidai zitabakia ndani na kuhatarisha afya zao, huku wakiomba wataalamu wa afya kupitia ofisi ya mganga mkuu kuwekeza nguvu ya utoaji elimu," amesema Mwampashi.
Kwa upande wake Diwani Viti maalumu, Vema Rungwe amesema matumizi ya kondomu za kike yana changamoto za ukubwa na pia hazitangazwi kwa jamii, ili kuleta uelewa kama inavyofanywa kwa kondomu za kiume.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ubatizo Songa amewataka wataalamu wa afya wilayani humo, kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike na kiume ili jamii iwe na uelewa wa kutosha. NMG