pmbet

Wanawake watakiwa kuachana na mikopo ya kausha damu

Eric Buyanza

December 21, 2023
Share :

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Dar es Salaam Janeth Masaburi,amewataka Wanawake wa wilaya ya Temeke waache kukopa mikopo ya kausha damu badala yake wakope mikopo inayotambulika na Serikali ikiwemo taasisi za fedha.
 

Mbunge Janeth Masaburi, alisema hayo jimbo la Temeke wakati wa kuzungumza na Mama lishe wa Temeke stereo, alipofanya ziara sokoni hapo na kuwapa elimu ya kutumia nishati mbadala na majiko ya gesi.
 

“Nawaomba wanawake wenzangu mchukue mikopo inayotambulika na Serikali, msichukue mikopo ya kausha damu mikopo hii wanawake inawaumiza riba yake kubwa”alisema Masaburi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet