Wanawake wengi wa Kenya wanatafuta pesa sio mapenzi - Mch Lucy
Eric Buyanza
April 23, 2024
Share :
Kutoka nchini Kenya, mchungaji Lucy Natasha ameelezea hofu yake kwa jinsi kasi ya wanawake wengi wa Kenya kufuata pesa kwa wanaume inavyoongezeka na kuwaonya wanaume kuwa waangalifu na wanawake wa aina hiyo.
Katika mahojiano na Oga Obinna, Natasha alisema wanawake hawapo tena kwenye mahusiano kwa ajili ya mapenzi bali kwa ajili ya pesa.
“Katika kizazi chetu wanawake wengi hawatafuti mapenzi, wanatafuta msaada, hawapendi moyo wako, wanapenda pesa zako, wakiingia kwenye uhusiano wanakuja kwa makusudi kwa kile wanachoweza kupata kifedha"
TUKO